November 24, 2024

Jinsi ya kuishinda hofu ya kupata chanjo ya Corona

Hofu hiyo inasababishwa na kusambaa kwa habari zisizo za ukeli juu ya chanjo za Corona zinazozua taharuki miongoni mwa watu.

  • Hofu hiyo inasababishwa na kusambaa kwa habari zisizo za ukeli juu ya chanjo za Corona.

Dar es Salaam. Utolewaji wa chanjo ya Corona ni miongoni mwa maeneo yaliyojaa habari za uzushi ikiwemo chanjo kuwa na madhara dhidi ya watu uku wengine wakihoji ufanisi wa chanjo zinazotolewa.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), tangu utolewaji wa chanjo ya Corona, hakuna chanjo ambayo imefanya kazi kwa asilimia 100 katika majaribio yake.

Lakini chanjo ambazo zimethibitishwa na WHO zimeonyesha ufanisi mkubwa wa kupambana na ugonjwa huo.

Kwa nini unashauriwa kuepuka hofu ya kupata chanjo ya Corona inayoendelea kusambazwa na watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii na tovuti? Fuatilia dondoo hizo muhimu kwa kutazama video fupi.