November 24, 2024

Vyakula anavyotakiwa kuepuka mwanamke wakati wa ujauzito

Mjamzito anashauriwa kutumia lishe bora kwa ajili yake na mtoto wake.

  • Ni pamoja na pombe, vyakula visivyooshwa na viungo vya wanyama.
  • Baadhi ya vyakula vina vimelea kama bakteria ambao wanaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto.

Dar es Salaam. Kipindi cha ujauzito ni kati ya vipindi ambavyo vinahitaji umakini kwa aili ya kumsaidia mama anayetarajia kujifungua ili amlete mtoto huyo duniani akiwa salama na pia mama abaki akiwa na afya njema.

Ili kuhakikisha afya ya mama na mtoto wake iko sawa, mjamzito anatakiwa kuzingatia lishe kwa kula vyakula vitakavyomsaidia yeye na mtoto wake kuwa na afya bora ikiwa ni ushauri baada ya kuonana na mtaalamu wa afya.

Mfano, mtaalamu wa afya anaweza kusema mama anahitaji damu ya kutosha hivyo atashauriwa vyakula gani vinavyoongeza damu viongezwe kwenye lishe yake.

Pia vipo vyakula ambavyo hashauriwi kuvitumia kabisa au anatakiwa kupunguza ikiwemo pombe na kahawa. Ni vyakula gani vingine anatakiwa kuepuka? Tazama video hii fupi kujifunza zaidi: