October 6, 2024

Huyu ndiye rafiki wa kweli wa mafanikio yako

Mtu huyo ni wewe ambaye unatakiwa kuwajibika na maisha yako binafsi bila kusubiri watu wengine wakushike mkono na kukupeleka kule unakotaka.

  • Mtu huyo ni wewe ambaye unatakiwa kuwajibika na maisha yako binafsi.

Katika maisha, kila mtu anatamani afikie ngazi fulani ya maisha. Iwe katika elimu, biashara au hata kazi, kunakuwa na matamanio fulani ya mtu kukua ili kufikia ndoto zake.

Ili mtu apande ngazi na kwenda kule anakotaka, anahitaji marafiki na watu wa karibu watakaomshika mkono na kumpa ‘support’ ya kila anachofanya. 

Lakini wote hao hawatakua na maana yoyote kama hauna rafiki mmoja mwenye umuhimu mkubwa ambaye ni UWAJIBIKAJI. Rafiki huyu ni wewe mwenyewe.

Unatakiwa kuwajibika na maisha yako binafsi bila kusubiri watu wengine wakushike mkono na kukupeleka kule unakotaka.

Uwajibikaji ni pamoja na kuwa na nidhamu, kutumia muda vizuri na kujikosoa pale unapofanya makosa na kufurahia kile unachokifanya na kukipa umuhimu unaostahili.

Anza leo kuwajibika kwa matendo yako. Kufahamu zaidi tazama video hii ambayo Mwandishi wa vitabu na mshauri wa masuala ya vijana, Neema Simbo anakujuza zaidi kuhusu dhana ya uwajibikaji.