November 24, 2024

Mbinu za kudhibiti mafamba ya chanjo ya Covid-19 kwa njia ya WhatsApp

Unashauriwa kupata habari zako kutoka kwa chanzo kinachoaminika.

  • Ni pamoja na kuepuka kusambaza ujumbe ambao hauna uhakika nao.
  • Pia kuepuka makundi sogozi ambayo yanakawaida ya kutuma habari za uongo.

Dar es Salaam. Kwa kuwa WhatsApp ni sehemu ya maisha ya watumiaji wa simu janja, mtandao huo pia umekuwa ni mojawapo wa nyenzo kuu za mawasiliano na utoaji wa taarifa kwa wengi.

Mtandao huo unaoruhusu mawasiliano binafsi na ya vikundi umekuwa ni mtandao muhimu kwa ajili ya kuwasiliana.

Hata hivyo, baadhi ya wapotoshaji hutumia WhatsApp kupotosha kwa kutuma habari zisizo na ukweli zikiwemo habari kuhusiana na chanjo za ugonjwa wa Corona.

Miongoni mwa habari hizo ni madhara na video za kuzua taharuki zinazohusiana na chanjo ya Corona na picha za kutishia watu zinazohusiana na ugonjwa wa Covid-19.

Unawezaje kuzuia usambaaji wa habari hizo (mafamba) zenye madhara kwa watu unaowasiliana nao? Tazama video hii kuepuka kuingia “mkenge”.