November 24, 2024

Ufanye nini unapokutana na habari kuhusuiana na chanjo ya Corona?

Habari isiyo ya ukweli inaweza kusababisha taharuki katika jamii endapo itaenea.

  • Inashauriwa kuhakiki uthabiti wa chombo cha habari ulichopata taarifa kuhusu chanjo ya Corona.

Dar es Salaam. Tangu mlipuko wa ugonjwa wa Corona, mitandao ya kijamii imekuwa ni jukwaa la watu kupata habari mbalimbali kuhusiana na ugonjwa huo. 

Pale chanjo ya Corona ilipotangazwa, bado watu wanatumia mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali za habari kupata habari za namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona ulichukua maisha ya watu zaidi ya milioni 3.6 ulimwenguni hadi sasa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). 

Hata hivyo, baadhi ya habari hizo zimekuwa siyo za ukweli na lengo la kuchapishwa ni kuzua taharuki miongoni mwa watu na kuongeza uoga miongoni mwa watu.

Pale unapokutana na habari kuhusiana na ugonjwa wa chanjo, yapo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuhakikisha uthabiti wa habari hiyo ikiwa ni pamoja na kukagua urasmi wa chombo kilichokuhabarisha.