October 6, 2024

Mambo ambayo mjamzito anashauriwa kuzingatia kuelekea kujifungua mtoto wa kwanza

Mama mjamzito anatakiwa kuondoa mzingira yote yatakayompa mawazo ikiwa ni pamoja na uhakika wa hospitali ya kujifungulia.

  • Ni pamoja na kuwa na uhakika wa hospitali atakayoenda kujifungulia.
  • Pia, kuandaa nyaraka muhimu ikiwemo bima ya afya na fedha za dharula.

Dar es Salaam. Kuelekea kujifungua, ni kati ya siku ambazo huwa ngumu kwa mama mjamzito ambaye ndio mara yake ya kwanza kujifungua. 

Baadhi huwa na mawazo ya jinsi hali itakavyokuwa na endapo watajifungua salama au la.

Hata hivyo, mawazo hayo yanaweza kupungua endapo mama amejiandaa inavyopaswa kuelekea siku yake ya kujifungua mtoto wake ajaye.

Mambo hayo ni pamoja na kuwa na bima ya matibabu pamoja na uhakika wa hospitali ipi ataenda kujifungulia.

Ni mambo gani mengine yatakayompa mama amani kuelekea siku yake ya leba? Tazama video hii kujifunza zaidi.