October 6, 2024

Ufanye nini kama unafanya kazi sehemu yenye vumbi?

Baada ya kufahamu eneo lako la kazi ni la vumbi, unashauriwa kuchukua tahadhari ikiwemo kufanya usafi wa mara kwa mara.

  • Unashauriwa kufanya usafi mara kwa mara.
  • Pia vaa barakoa kwa ajili ya kujikinga na vumbi hilo.

Dar es Salaam. Ni vigumu kuchagua mazingira ya kazi hasa kwa waajiriwa. Kwa walio na bahati, hupata kazi katika mazingira mazuri, wengine hupata kazi katika mazingira tulivu na wengine hujikuta katika mazingira ambayo siyo rafiki kiafya yakiwemo yenye kelele na vumbi.

Mazingira yenye  vumbi yanaweza kuwa chanzo cha matatizo kiafya ikitegemeana na aina ya vumbi ambalo  mtu anafikiwa nalo. Mfano kwa vumbi la udongo huweza kuwa chanzo cha mafua na kwa wengine kusababisha changamoto za upumuaji.

Kwa mujibu wa tovuti ya hasbod.com, aina zingine za vumbi ikiwemo vumbi la mbao na vumbi linalotokana na baadhi ya kemikali ikiwemo “sillica” na nyuzi za “Asbestos”, zinaweza kuwa sababu ya saratani kwa mtu anayefikiwa na vumbi hilo.

Kupambana na hali hiyo, inashauriwa kuvaa vifaa vya kujikinga ikiwemo nguo maalumu na miwani na pia kusafisha ofisi yako mara kwa mara. Ni njia gani zingine? Tazama video hii kujifunza zaidi: