Jinsi vijana wanavyoweza kuachana na tabia hatarishi
Njia ya kuzishinda tabia hizo kufahamu tatizo liko wapi na kuanza kujielekeza katika mambo yenye manufaa.
- Baadhi ya tabia zinafananishwa na ulevi kwa sababu zinaharibu maisha ya mtu.
- Njia ya kuzishinda tabia hizo kufahamu tatizo liko wapi na kuanza kujielekeza katika mambo yenye manufaa.
Dar es Salaam. Wengi wetu tumezoea kuona watu wakinywa pombe kwa kupitiliza na tunawaita walevi. Lakini hatufahamu kuwa ulevi ni zaidi ya kunywa pombe.
Huenda watu wote ni walevi lakini wanatofautiana katika mambo yanayowafanya walewe na kufanya baadhi ya mambo kwa kupitiliza na kuathiri maisha yao ya kawaida.
Wewe ulevi wako uko katika nini? Wapo ambao wanatumia simu kupita kawaida, kucheza michezo ya mtandaoni, kupenda mpira, kamali na hata kupiga umbea na bado wakasema wao siyo walevi.
Siyo vibaya kufanya unachokifanya lakini una kiasi nacho au ndiyo kimekufanya ushindwe kufanya mambo mengine na kutumia muda mrefu kukifanya huku kikurudisha nyuma katika mchakato wa kujenga maisha bora.
Mtu anapokuwa mlevi wa jambo hujikuta anashindwa kujizuia na lile jambo ama hicho kitu kinakuwa sehemu ya maisha yake na anaweza akawa anajua ama hajui kabisa maana ni kawaida mwili umezoea na akili imezoea na maisha yake ndiyo yalivyo na watu waemzoea hivyo.
Bado una nafasi nzuri ya kuachana na ulevi wako na ukarejea katika maisha ya kawaida. Hatua ya kwanza, fahamu kuwa una ulevi yaani kuna tatizo.
Tafuta mbinu au njia mbadala zitakazokufanya kuchukia jambo unalofanya sasa na anza kujielekeza katika masuala ya msingi yenye faida kwako.
Inaweza kuwa ngumu kuachana na hiyo tabia lakini ukidhamiria kwa dhati unaweza kubadilika. Tazama video hii kujifunza zaidi: