Lugha unayozungumza inaeleweka kwenye jamii?
Tafuta watu ambao mnaweza kuzungumza lugha ambayo mtaelewana.
- Tafuta watu ambao mnaweza kuzungumza lugha ambayo mtaelewana.
Dar es Salaam. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na makabila zaidi ya 100 ambayo yanazungumza lugha tofauti. Lakini lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya Taifa inayotuunganisha katika shughuli mbalimbali.
Kiswahili kimeondoa matabaka ya watu fulani kujiona ni wa thamani kuliko watu fulani na hivyo kujenga jamii yenye mshikamano na utengemano wa makabila yenye lugha tofauti.
Leo tunaangalia lugha katika mtazamo wa tofauti hasa kwa vijana ambao wanataka kufika mbali katika maisha. Wanatakiwa kutembea au kujihusisha na watu wanaozungumza lugha moja.
Hiyo ni maana kuwa watembee na watu ambao wanaowaelewa, wanaotambua na kuthamini kile wanachokifanya katika maisha yao. Kifupi hao ni watu wenye lugha moja na wewe.
Kama ilivyo katika mawasiliano, ukiongea na mtu ambaye lugha zenu ni tofauti, hamuwezi kuelewana na hata mnayopanga hayatafanikiwa.
Wewe unaishi na watu wa lugha gani? Hao ulionao wanaitambua kwa ufasaha lugha unayozungumza? Wanachokizungumza kinakufanya usonge mbele kimaisha?
Tathmini leo lugha unayozungumza na watu wako wa karibu. Tafuta watu ambao mnaweza kuzungumza lugha ambayo mtaelewana na itawafanya kuwa na malengo yanayofanana ili mfike kule mnakotaka kwa wakati.
Kufahamu zaidi, tazama video hii: