October 6, 2024

Watendaji wabadhirifu wizara ya ujenzi waonywa

Serikali imesema itawachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya umma.

  • Ni wale watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
  • Waziri wa Chamuriho amesema wanachelewesha miradi ya maendeleo.

Mwanza. Serikali imesema itawachukulia hatua  watumishi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya umma. 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akiwa jiji Mwanza leo Mei  3, 2021  amesema wapo watendaji  ndani  ya wizara hiyo wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha miradi ya maendeleo kutokamilika kwa wakati. 

Dk Chamuriho amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua watumishi hao. 

“Nitumie nafasi hii kuwataka watumishi kufanya kazi  kwa weledi wa kazi zao na kwa kufuata misingi na maadili ya utumishi wa umma,” amesema  Waziri Chamuriho.


Zinazohusiana: 


Amesema sekta ya ujenzi  ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi na hivyo umakini wa watendaji wake unahitajika zaidi. 

“Kabla ya mwaka wa fedha 2020/2021 kukamilika Serikali itahakikisha inakamilisha miradi yote iliyokuwa imepangwa katika mwaka huu wa fedha,” amesema

Afisa Ugavi Mwandamizi sekta ujenzi, Rehema Lingo amehidi kutekeleza maelekezo ya waziri ili kuhakikisha wanasaidia katika ukuaji wa uchumi huku akiwataka watendaji kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa na Serikali kukamilisha miradi yote inchini.