November 24, 2024

Jinsi ya kudhibiti nywele kupotea kichwani katika umri mdogo

Kula mlo kamili, epuka matumizi ya vifaa vya kukaushia nywele na matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara.

  • Ni pamoja na kuepukana na vifaa vya moto kichwani ikiwemo pasi za nywele.
  • Pia kuwa makini na mitindo ya nywele ambayo unachagua.

Dar es Salaam. Kupata uwalaza au kipara siyo jambo geni wala jambo la ajabu kwa watu ambao umri wao umeenda. Licha ya kuwa ni kitu cha kawaida kwa wanaume, baadhi ya wanawake pia hufikiwa na hali hiyo.

Tuvuti ya afya ya Healthline, imeandika kuwa, asilimia 50 ya wanawake wanapata uwalaza pale umri wao unapoenda huku wanaume wengi (asilimia 85) wakipata uwalaza pale wanapoingia miaka ya 50. 

Hata hivyo, healthline imesema lipo kundi la watu ambao wanapata uwalaza pale wanapoingia miaka yao ya 20 na hiyo husababishwa na mfumo wa vinasaba (DNA), mitindo ya kusuka nywele na msongo wa mawazo.

Ili kuepukana na changamoto hiyo, tazama video hii kujifunza.