Njia za kupata wateja wanaojirudia katika biashara yako
Inaweza kuwa ni kwa njia ya zawadi, kuwajulisha pale bidhaa na huduma mpya zinapoanzishwa au kutoa bidhaa na huduma bora kila siku.
- Ni pamoja na kuwapatia wateja wako zawadi. inaweza kuwa ofa, ua, kadi na chochote cha kufurahisha mioyo yao.
Dar es Salaam. Katika biashara hakuna jambo jema kama unavyokuwa na wateja wenye upendo wa dhati na biashara yako. Wateja wa aina hii wanaoijirudia huja mara kwa mara kununua huduma na bidhaa.
Wateja hawa huamini zaidi huduma na bidhaa zako na kuzitetea hata pale unapokuwa umejikwaa iwe ni vitabu, chakula, burudani, viatu nakadhalika.
Mteja ambaye amekuchagua wewe tu kumpatia huduma hiyo, ni mteja ambaye anahitaji umakini kwa kuwa ukimpoteza kumpata mwingine kama huyo huchukua muda mrefu.
Mpishi wa keki kutoka Kinyerezi jijini Dar es Salaam Oscar Busanji ameiambia Nukta habari (www.nukta.co.tz) kuwa mteja ambaye anajirudia ana thamani kubwa kwa kuwa ndiye anayepeleka jina lako kwa wateja wengine na kukupatia wateja wengi zaidi.
Hata hivyo, kwa baadhi ya wafanyabiashara, wanashindwa kuelewa thamani ya mteja huyo na kumhudumia kimazoea na hata kupunguza ubora wa huduma kwa kuwa wamemzoea.
Mjasiriamali kutoka Dodoma, Magdalena Mandawa anasema endapo utashindwa kumhudumia mteja huyo kwa upendeleo, atakukimbia siku atakapopata huduma bora zaidi.
Je, kama mfanya biashara, ni mbinu zipi unazoweza kuzitumia katika kumlinda na kuendela kumpata mteja anayejitudia? Tazama video hapo juu au fuatilia dondoo hapa chini.
Soma zaidi:
- Biashara ya juisi inavyowatoa kimaisha wasomi waliokataa kuajiriwa
- Binti aliyejisomesha kwa biashara za mitumba, viungo vya vyakula
- Maduka ya simu Makumbusho yaibua mjadala mpana wa bei, ubora
Njia za kupata wateja wanaojirudia katika biashara yako
- Hakikisha kiwango cha ubora cha huduma yako hakishuki bali kinapanda kila siku.Kuwa mbunifu kwa kila huduma au bidhaa unayoitoa.
- Jitahidi kuwa wateja wako wanapata bidhaa au huduma hiyo wakati wote.
- Wapatie wateja wako wanaojirudia zawadi. Siyo lazima ikawa mali. Inaweza kuwa kadi, ua, ofa na chochote cha kugusa moyo wao.
- Orodhesha wateja wako ambao wanajirudia na tengeneza utaratibu wa kuwakumbusha juu ya huduma zako na kuwahabarisha juu ya huduma mpya.
- Msome mteja wako kufahamu njia nzuri za kuwasiliana naye, wengine hukerwa na simu zako za kuwajulisha bidhaa na huduma zako.