October 6, 2024

Unavyoweza kuepuka maambukizi ya Corona kupitia barakoa

Iwapo hautafuata vema masharti ya uvaaji barakoa ikiwemo kufua mara kwa mara zile za vitambaa upo hatarini kupata virusi vya corona.

  • Ni kwa kuzingatia kanuni muhimu za matumizi ya  barakoa ikiwemo namna ya kuzitupa na kuzihifadhi.

Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) wameshauri  matumizi sahihi ya barakoa kama njia ya kujikinga na maambukizi ya Corona pale unapokuwa katika maeneno yaliyo na mkusanyiko na watu.

Hata hivyo, endapo barakoa haitotumika vizuri ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa moja kwa muda mrefu bila kufua au kuchangia barakoa na mtu mwingine inaweza kukupatia maambukizi.

Kupitia video hii, unaweza kujifunza njia mbalimbali za kuepuka maambukizi ya Corona pale unapokuwa unatumia barakoa.