November 24, 2024

Hakuna uthibitisho wanaotumia chanjo ya Corona kufariki dunia

Watu watakiwa kupata taarifa za chanjo ya Corona kutoka vyanzo vya kuaminika.

  • Baadhi ya watu hasa nchini Marekani wanawatisha watu kuwa akitumia chanjo hiyo watapoteza maisha.
  • Mpaka sasa mamlaka za afya hazijaongelea madhara yotokanayo na chanjo ikiwemo vifo. 
  • Watu watakiwa kupata taarifa za chanjo ya Corona kutoka vyanzo vya kuaminika.

Dar Es Salaam. Moja ya njia zinazotumika na nchi mbalimbali duniani kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, ni kutoa chanjo. Tayari jumuiya ya kimataifa imeanzisha kampeni ya kuwafikia watu katika maeneo yao ili kuwakinga dhidi ya virusi hivyo. 

Baadhi ya watu wenye nia mbaya wanaeneza uzushi katika mitandao ya kijamii kuwa chanjo dhidi ya Corona haifai kwa sababu ina madhara ikiwemo kusababisha vifo kwa wanaopata. 

Hivi karibuni kumekuwa na uzushi mwingi kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Whatsapp pamoja na tovuti ya Irish Sentinel kwamba madhara ya chanjo yameanza kuonekana duniani baada ya daktari kutoka hospitali ya Wexford nchini Uingereza kufa baada ya kupata chanjo ya Corona.

Taarifa hiyo inayosambaa mitandaoni inasema daktari wa miaka 39 ambaye ni  mtoto wa Jaji Mkuu wa Marekani amekutwa amekufa siku chache baada ya kupata chanjo nchini Marekani.

Taarifa hiyo inayosambaa mitandaoni ikiwa na picha ya daktari huyo kutoka tovuti ya Health Impact News inasomeka “39 -Year-Old Medical Doctor and Son of Former Chief Justice of Trinidad Founded Dead After COVID Injection in Ireland,” 

Kipande hicho kinamaanisha kuwa “Daktari wa miaka 39 na mtoto wa Jaji Mkuu amekufa baada ya kupata chanjo ya Corona Ireland”. Hata hivyo hakuna uthibitisho juu ya kifo hicho.

Pia taarifa hizo za uzushi zimewahusisha watu mbalimbali wakiwemo madaktari nchini humo kuwa wanafariki mara baada ya kupata chanjo, jambo ambalo siyo sahihi. 


Zinazohusiana:


Taarifa hiyo na zingine siyo za kweli kwa sababu hakuna ripoti yoyote iliyotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) au mamlaka yoyote rasmi inayohusiana na masuala ya afya kuwa chanjo ya Corona inaleta madhara au kuua.

Taarifa zote juu ya matokeo yanayosababishwa na chanjo hizo zinapaswa kutoka mamlaka zinazohusika ili kutoa taarifa zilizo na ukweli na rasmi.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanashauriwa kufuatilia taarifa na machapisho kutoka vyanzo vinavyoaminika ikiwemo WHO ili kupata taarifa zenye ukweli.