November 27, 2024

Umuhimu wa kutenda mema kwa watu wanaokuzunguka

Dunia inahitaji wema wako hata kama ni mdogo kiasi gani kwa sababu unachangia kuifanya dunia kuwa sehemu ya kuishi.

  • Dunia inahitaji wema wako hata kama ni mdogo kiasi gani kwa sababu unachangia kuifanya dunia kuwa sehemu ya kuishi. Pia unaongeza furaha na amani. 

Siku ina saa 24 tu na ina mengi sana ndani yake yanayoonekana na yasioonekana. Yapo mazuri na mabaya. Wewe umechagua kufanya mabaya au mazuri?

Katika maisha ya kila siku, kila mtu ana mapambano yake na ana namna yake kupambana ili kufikia hatma yake. Lakini hilo halimzuia kuwa mtu mwema anayetenda mema kwa wengine/.

Katika huu ulimwengu uliojaa changamoto mbalimbali za kimaisha,  chagua kuwa mtu mzuri, chagua kutenda wema na mkarimu kwa wanaokuzunguka. 

Dunia inahitaji wema wako hata kama ni mdogo kiasi gani kwa sababu unachangia kuifanya dunia kuwa sehemu ya kuishi. Pia unaongeza furaha na amani. 

Matendo mema hayako mbali sana wala hayana gharama ni mambo yalio ndani ya uwezo wako  ni jambo la kuamua tu  na kutumia hekima.

Mathalan, kauli yako njema kwa jirani yako ya kumwambia “unamtakia siku njema” au unampenda” ni faraja tosha kwake kumfanya ajisikie salama na jamii iko upande wake. 

Kama wema wako unaruhusu kwenda zaidi ya maneno, basi watendee yaliyo mema wanaokuzunguka hata kama ni adui zako. Wape chakula namavazi wenye uhitaji. Washauri kwa busara wanaokwenda katika njia zisizostahili. 


Soma zaidi:


Hata hivyo, baada ya kutenda wema, usisubiri kusifiwa au kupongezwa. Ndiyo maana kuna usemi unaosema “tenda wema, nenda zako”. Tenda wema hata kama hakuna anayekuona au atakayekupongeza.

Tabia hiyo ya kutenda mema huenda ikakufungulia fursa mbalimbali kwenye maisha ikiwemo kupendwa na watu na hata kusaidiwa ukipata matatizo kwenye jamii. 

Pia unaweza kupata watu watakaokulia siku ukiondoka duniani. Jiulize mara ya mwisho kutenda au kutoa maneno mema kwa rafiki, jirani au ndugu yako ilikuwa lini?

Kama haujawa mwema kwa wenzako, bado una nafasi ya kuanza upya leo. Anza kwenye familia yako, kwa majirani na hata watu usiowajua watendee wema. 

Usiwe mwepesi wa kutenda mabaya kwa sababu hakuna anayefahamu kesho yake itakuaje.

Kufahamu zaidi jinsi unavyoweza kuwa mwema, tazama video hii: