October 7, 2024

Haya ndiyo utakayokutana nayo unapofanya biashara mtandaoni

Ni pamoja na kuuziwa bidhaa feki kwa bei kubwa na kupata kitu tofauti na picha uliyoiona.

  • Wafanyabiashara za mtandaoni wanashauriwa kuwa wakweli ili kuwapatia wateja wao wepesi wa kufanya maamuzi.

Dar es Salaam. Mitandao ya kijamii siyo tu inatumika kwa mawasiliano baina ya watu, bali ni jukwaa muhimu kwa watu kufanya biashara ili kujiletea maendeleo.

Kwa sasa, mtu ana uwezo wa kuingia Instagram, facebook, Twitter na hata WhatsApp na kutafuta bidhaa anayohitaji na hivyo kufanya maamuzi ya kuinunua.

Hata hivyo, kufanya biashara mtanaoni, kumeambatana na changamoto kadhaa ikiwemo kukosa uaminifu na hivyo kupoteza wateja.

Nukta imekusanya maoni na mapendekezo ya kuwasaidia wafanyabiashara wa mtandaoni kuboresha huduma zao na haya ndiyo matokeo.