October 7, 2024

Jinsi kitafutio cha Google kinavyoweza kukupatia taarifa sahihi za COVID-19

Kikitumika vizuri kinaweza kukupatia taarifa sahihi na kukuondolea mashaka ya uzushi wa COVID-19.

  • Kitafutio hicho ni bidhaa ya kampuni ya Google inayosaidia kupata vitu mbalimbali mtandaoni.
  • Kikitumika vizuri kinaweza kukupatia taarifa sahihi na kukuondolea mashaka ya uzushi wa COVID-19.

Dar es Salaam. Dunia inaenda kasi hasa katika ukuaji wa teknolojia ya upashanaji habari. Maisha yamekuwa mepesi kwa sababu taarifa zozote unazohitaji utazipata kwenye kiganja cha mikono yako.

Kwa kutumia simu janja yenye programu za vitafutio vitu mtandaoni ikiwemo “Google Search” unaweza kupata kila kitu bila kunyanyua mguu wako kutafuta taarifa kwenye ofisi za Serikali au masharika mbalimbali.

Kitafutio hicho ambacho kitakupata habari kwa namna tofauti zikiwemo picha, ramani, vitabu, nyaraka za sauti, maandishi au video, pia ni nyenzo muhimu ya kupoata taarifa sahihi kuhusu janga la Corona linaloitesa dunia kwa sasa.


Kama unataka kufahamu chochote kinachoendelea kuhusu COVID-19 unaweza kutafuta neno hilo ambalo utapata majibu ya machaguo mbalimbali na kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi ya juu ya kujikinga na ugonjwa huo. 


Pia ipo sehemu ya picha na video ambapo utapata taarifa za picha mbalimbali kuhusu ugonjwa huo ambazo zimepigwa au kutengenezwa katika maeneo mbalimbali duniani.

Pia sehemu nyingine ambayo huwa haitumiwi na watu wengi ambayo inaweza kukupa matokeo mazuri kwenye kitafutio hicho ni sehemu ya zana (tools) ambapo zinatoa majibu mbali ya muda ambao habari imechapishwa, aina ya nyaraka unazohitaji.


Hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini wakati huu dunia inapambana na janga la Corona kwa kutosambaza habari zisizo sahihi na kutumia kifatutio cha Google katika kupata habari sahihi hasa wanapokutana na habari wanayoitilia mashaka.