October 7, 2024

Faida utakazozipata ukichukua tahadhari dhidi ya Corona mapema

Itakusaidia kuwa salama na kukuepushia gharama kubwa za matibabu endapo utapata ugonjwa huo.

Dar es Salaam. Huenda bado unasubiria jirani yako aanze kuvaa barakoa kisha na wewe ndiyo ufanya hivyo au unasubiri hadi uone ndoo za kunawia kwa majirani zimewekwa na wewe ndiyo ufanye hivyo. 

Kama wewe upo katika kundi hilo, unahitaji kujitafakari.

Kwa kupuuza tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona, huenda ukawa katika hatihati ya kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao unasumbua mataifa mengi duniani.

Hata hivyo, endapo utachukua tahadhari mapema dhidi ya ugonjwa huo, unaweza kujiweka salama zaidi dhidi ya ugonjwa huo na kuwalinda unaowazunguka.

Kufahamu zaidi, tazama video hii