November 24, 2024

Shule 10 bora kidato cha nne mwaka 2020 hizi hapa

Shule ya Wasichana ya St Francis ya mkoani Mbeya yaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa.

  • Shule ya Wasichana ya St Francis ya mkoani Mbeya imeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
  • Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaingiza shule tatu kila moja. 

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato nne mwaka 2020 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri huku Shule ya Wasichana ya St Francis ya mkoani Mbeya ikishika nafasi ya kwanza kitaifa.

St. Francis imepanda kutoka nafasi ya pili iliyoshika mwaka juzi na kuishusha Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera hadi nafsi ya nne.  

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa  leo (Januaria 15, 2021), Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amezitaja shule nyingine zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo kuwa ni  Iliboru ya mkoani Arusha, Cannosa (Dar es Salaam), Kemebos (Kagera) na  Feza Boys ya jijini Dar es Salaam.

Nyigine ni Ahmes, St Aloysius Girls, Marian Boys (Pwani) na St. Augustine Tagaste ya jijini  Dar es Salaam. 


Soma zaidi: 


Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam imefanikiwa kuingiza shule tatu kila moja katika orodha hiyo ya dhahabu, huku

Katika orodha hiyo, Serikali imefanikiwa kuingiza shule moja tu ya Ilboru huku zilizobaki zikiwa ni shule binafsi. 

Kupata matokeo ingia hapa >>>>> https://bit.ly/2XIyOu0