November 24, 2024

Fanya haya kuepuka kufungiwa akaunti zako za mitandao kijamii

Ni pamoja na kua na uhakika na chanzo cha taarifa zako unazosambaza kwa wenzako.

Dar es Salaam. Kutokana na taharuki, kutaka kuwalinda uwapendao na hata kuwa msamalia mwema, huenda umewahi kutaka kutuma ujumbe unaohusu Corona ambao hauna uhakika nao. 

Usilolijua ni kuwa, kwa sasa mitandoa ya kijamii ikiwemo Instagram, Youtube na Facebook imeweka sheria kali dhidi ya kusambaza taarifa za uzushi kuhusu ugonjwa huo.

Mathalan, mtandao wa kupakia habari video wa YouTube hutoa onyo pale mtu anapokuwa anataka kutuma maudhui yanayohusiana na ugonjwa wa Corona na kisha kutoa adhabu ya kufungiwa kwa wiki moja au zaidi ikiwa atajaribu kuweka maudhui yasiyofaa.

Ili kuepukana na kufungiwa mitandao yako ya kijamii, unahitaji kuwa makini kwa kuthibitisha habari zako kwa kutumia zana za kidijitali zikiwemo TinEye na Google reverse Image.

Kufahamu zaidi, tazama video hii.