November 24, 2024

Faida za kuishi karibu na sehemu ya kazi

Mbali na kuokoa gharama za usafiri, huenda ikakurahisishia kupata chakula kizuri cha nyumbani.

  • Mbali na kuokoa gharama za usafiri, huenda ikakurahisishia kupata chakula kizuri cha nyumbani.
  • Kama mzazi, itakupatia nafasi ya kushiriki katika malezi ya watoto wako ikiwemo kuwasaidia kazi za shuleni.
  • Kama bachela, huenda ikakupa urahisi wa kufika nyumbani mapema na kupata muda wa kupumzika.

Dar es Salaam. Ili kufahamu kwanini habari hii imeandikwa, fikiria huwa unatumia muda gani kusafiri kutoka nyumbani kwako hadi kufika eneo lako la kazi?

Wapo wanaotumia saa matatu na hivyo kufika nyumbani kwao saa tatu usiku licha ya kutoka kazini saa 11 jioni.

Kama wewe ni mmoja wa watu hao, huenda ukakubaliana na ukweli kuwa gharama unazozitumia huenda ungelizitumia kufanya maendeleo mengine yakiwemo kukuongezea vyanzo vya kipato.

Mathalani, kama unatumia Sh50,000 kwa wiki kwa ajili ya gharama za mafuta, fedha hiyo ni sawa na Sh200,000 kwa mwezi na Sh2.4 milioni kwa mwaka ambayo huenda inafaa kuwa mtaji wa biashara au kulipia kodi eneo la karibu na kazini kwako.

Ni mawazo tu! Lakini hizi ni baadhi ya faida nyingine utakazozipata kwa kuishi karibu na eneo lako la kazi. Tazama video hii: