October 7, 2024

Namna uzushi kuhusu Corona unavyosambaa kwenye mtandao wa WhatsApp

Huanza na mtu mmoja ambaye hutuma ujumbe kwa rafiki akiwa na lengo la kumkinga na ugonjwa wa Corona kisha husambaa kwa watu wengi.

  • Huanza na mtu mmoja ambaye hutuma ujumbe kwa rafiki akiwa na lengo la kumkinga na ugonjwa wa Corona.
  • Ujumbe huo huendelea kusambaa pale mtu aliyetumiwa anaamua kuusambaza kwa wengine.
  • Taharuki huibuka na kusababisha watu kufanya maamuzi magumu.

Dar es Salaam. Kama unatumia simu kusoma makala hii fupi, bila shaka ni mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa WhatsApp na mara nyingi umekutana na ujumbe kuhusu virusi vya COVID-19.

Jumbe hizo ambazo husambaa zaidi katika makundi sogozi (groups) ya mtandaoni humo huwa sababu ya taharuki kwa wengi na kuwafanya watu kukosa amani na maisha kwa kuchukua maamuzi magumu.

Tazama video hii kujifunza zaidi.