Hii ndiyo tiba sahihi ya magonjwa ya moyo
Ni pamoja na kufanya mazoezi walau mara tatu kwa wiki. Pia kuwa mwangalifu na chakula na vinywaji unavyotumia kila siku.
- Ni pamoja na kufanya mazoezi walau mara tatu kwa wiki.
- Pia kuwa mwangalifu na chakula na vinywaji unavyotumia kila siku.
- Endapo uzito wako umepitiliza, jitahidi kuupunguza kwa kufuata ushauri wa waaalamu.
Dar es Salaam. Ugonjwa wa moyo ni kati ya maradhi yanayowasumbua watu wengi duniani.
Sababu kubwa inayotajwa kusababisha matatizo ya moyo ni mtindo mbaya wa maisha ikiwemo ulaji wa chakula usiozingatia kanuni bora za lishe.
Yapo baadhi ya mambo ambayo ukifanya yatakusaidia kuepuka changamoto za kiafya kwenye kiungo hicho muhimu mwilini ikiwemo kufanya mazoezi na kuepuka unywaji wa pombe uliopitiliza.
Je, ni mambo gani mengine ya kuzingatia ili kuepukana na maradhi ya moyo? Video hii inakufahamisha zaidi.