Zaidi ya nusu ya wagonjwa wa Corona wapona Afrika
Hadi jana Desemba 4, 2020 bara hilo limeripoti visa milioni 2.3.
![](https://cms.nukta.co.tz/wp-content/uploads/2021/03/bcb79b81018eca6c30031462039b2984.jpg)
Dar es Salaam. Wakati wagonjwa wa Corona wakiendelea kuongezeka Afrika, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinazonyesha kuwa zaidi ya nusu ya wagonjwa wanaopata COVID-19 wamepona barani humo.
Takwimu za WHO za Desemba 4, 2020, zinaonyesha watu waliopona COVID-19 barani humo ni milioni 1.8 kati ya wagonjwa milioni 2.3 walioripotiwa kupata maambukizi.
Hata hivyo, nchi ya Afrika Kusini imeendelea kurekodi kiwango cha juu cha wagonjwa wa COVID-19 barani humo.