November 24, 2024

Programu hii inavyopambana na habari za uzushi kuhusu Corona

Teknolojia hii itakusaidia kung’amua habari picha za uzushi kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Dar es Salaam. Mara nyingi pale matukio kama mlipuko wa ugonjwa wa Corona yanapotokea, ndipo picha zinazohusiana na matukio hayo zinapoanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii huku zikisababisha taharuki na hofu kwa watu wanaofikiwa nazo.

Mfano wa picha hizo ni matukio ya mwisho wa dunia, watu kufa kikatili katika mitaa mbalimbali, milipuko ya majengo na nyingine ambazo huenda zikakupatia taharuki itakayokuachia maumivu. 

Hata hivyo, wakati mwingine picha hizo huwa siyo za kweli na haziendani na tukio lililotokea kwa wakati huo kwani baadhi huwa ni picha kutoka kwenye filamu, zingine zikiwa ni picha zilizotengenezwa kwa malengo fulani.

Utawezaje kung’amua picha hizo? Simu yako ya mkononi tu inakutosha. Tazama video hii kujifunza.