Umuhimu wa matangazo ya kidijitali kwa wafanyabiashara
Ni pamoja na kumpatia mfanyabiashara takwimu halisi za kiwango cha kusambaa na usomekaji wa tangazo.
- Ni pamoja na kumpatia mfanyabiashara takwimu halisi za kiwango cha kusambaa na usomekaji wa tangazo.
- Pia, humsaidia mfanyabiashara kupata mrejesho juu ya biashara yake kupitia mitandao ya kijamii.
- Yanatoa fursa ya kufanya uchambuzi juu ya watu waliovutiwa na bidhaa au huduma.
Dar es Salaam. Kama mfanyabiashara unatumia nini kutangaza biashara yako?
Iwe vipeperushi, matangazo ya redio na televisheni, bila shaka lengo lako ni kuwafikia wateja wengi zaidi ili kuikuza biashara yako.
Wataalam wa masoko wanashauri wafanyabiashara kuwekeza katika matangazo ya kidijitali kwa sababu ni rahisi kupata takwimu halisi za kiwango cha kusambaa kwa tangazo husika.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya masoko ya kidijitali ya Mayocoo, Justice Donatus amesema, kutangaza kidijitali kutakupatia takwimu halisi na hata mrejesho kutoka kwa wateja wako juu ya biashara yako.
“Ukisema uweke tangazo lako barabarani, hauwezi kujua ni wangapi wamesoma, ni wangapi wamechukua hatua ya kutembelea tovuti au mitandao ya kijamii ya kampuni au biashara yako,” amesema Donatus.
Mtaalamu huyo amesema endao mtu akitangaza kidijitali mfano kwa njia ya Instagram, anaweza kuona watu waliofikiwa na tangazo, waliofurahia tangazo hilo na kuchangamana nalo na hata waliochukua hatua ya kutembelea ukurasa wa kampuni ili kujua zaidi kuhusu biashara yako.