November 24, 2024

Ufanye nini unapopokea ujumbe kuhusu COVID-19 kwa njia ya WhatsApp?

Ni pamoja na kutokutuma habari unayoipata bila kuithibitisha

Dar es Salaam. Mtandao wa WhatsApp ni kati ya mitandao inayotumiwa na watu wengi duniani huku takwimu zikitaja mtandao huo kutumiwa na watu zaidi ya bilioni 1.5 duniani. Hayo ni mafanikio makubwa ya kiteknolojia.

Hata hivyo, ni miongoni mwa mitandao ya kijamii ambayo hutumiwa na watu kusambaza habari za uzushi kuhusu Corona. 

Kama wewe ni miongoni wa watumiaji wa mtandao huo, una nafasi nzuri ya kukabiliana na habari za uzushi kwa kuongeza umakini kila unapopokea habari. 

Ufanye nini unapokutana na ujumbe wa aina hiyo? Tazama video hii: