November 24, 2024

Jinsi ya kuripoti habari ya uzushi kuhusu Corona katika mtandao wa Facebook

Mtandao huo ukigindua taarifa ni ya uongo unazuia usisambazwe kwa watu

  • Mtandao huo umeweka mfumo maalum wa kuripoti taarifa zote za uzushi kuhusu Corona.
  • Mtandao huo ukigindua taarifa ni ya uongo unazuia usisambazwe kwa watu.

Dar es Salaam. Wakati jitihada za kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona zikiendelea duniani bado kumekuwa na wimbi kubwa la usambazaji wa taarifa potofu na za uongo kuhusu ugonjwa huo katika mitando ya kijamii ikiwemo Facebook.

Hali hiyo, imeiwezesha Facebook kuanzisha mfumo maalum unaosaidia kukabiliana na taarifa za uzushi kuhusu COVID-19 ili kuwalinda watumiaji wake wasipate madhara zaidi.

Mfumo huo pia unawawezesha watumiaji wa mtandao huo unaokua kwa kasi kuthibitisha na kuripoti taarifa anayofikiri siyo ya kweli kuhusu janga la Corona.  

Kwa mujibu wa Facebook, hatua ya kwanza ya kuripoti taarifa ya uzushi ni kwenda kwenye alama yenye nukta tatu zinazopatikana upande wa juu wa kulia wa ukurasa wa mtandao huo.


Zinahusiana:


Hatua ya pili utatakiwa kubonyeza hizo nukta tatu kisha unaenda kwenye kipengele cha mwisho kabisa cha “Find support” (tafuta msaada)  or “report post”  na kisha utapata kipengele kingine cha “Fake News” (Habari za uzushi).

Katika kipengele hicho, ndipo unapoweza kulipoti taarifa ya COVID-19 unayofikiri ni ya uzushi.

Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Corona duniani, ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake.