October 7, 2024

Corona bado yaitesa dunia

Ugonjwa huo umeua watu zaidi ya milioni 1.3.

  • Ugonjwa huo umeua watu zaidi ya milioni 1.3.
  • WHO yasisitiza watu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo. 

Dar es Salaam. Wakati chanjo ya Corona (COVID-19) ikiendelea kufanyiwa utafiti, Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za hadi Novemba 16, 2020 zinaonyesha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yamefikia visa milioni 54.3 huku zaidi ya watu milioni 1.3 wakipoteza maisha. 

WHO inasisitiza watu kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara na kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya.