October 7, 2024

Unayopaswa kuzingatia kabla ya kununua bidhaa za watoto

Baadhi ya bidhaa zikiwemo pafyumu zenye harufu kali huwafanya watoto kupata mafua na kushindwa kupumua vizuri.

  • Ni pamoja na kuwa makini katika kusoma maelekezo yaliyoandikwa kwenye bidhaa ambayo unanunua.
  • Epuka kununua bidhaa zenye harufu kali ili kumuepusha mtoto na matatizo ya mfumo wa upumuaji. 
  • Muone mtaalam wa afya akupe maelekezo ya baadhi ya bidhaa zitakazomfaa mtoto wako.

Dar es Salaam. Huenda mtoto wako anakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya pasipo kujua chanzo chake. Matumizi ya baadhi ya bidhaa za ngozi yakiwemo mafuta yenye harufu kali ni sababu mojawapo. 

Baadhi ya bidhaa zikiwemo pafyumu zenye harufu kali huwafanya watoto kupata mafua na kushindwa kupumua vizuri. 

Kwa mujibu wa tovuti ya parenting.firstcry.com inayojihusisha na masuala ya watoto, malashi makali ya mzazi na hata yalipo kwenye bidhaa za mtoto yanaweza kumsababishaia mtoto changamoto kwenye mfumo wa upumuaji.

Ili kumuweka salama mtoto wako, tazama video hii kujifunza mambo ya kuzingatia wakati unanunua bidhaa za ngozi kwa ajili yake.