Bei ya viazi mviringo haikamatiki Mtwara
Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoa wa Mtwara linauzwa kwa Sh110,000, wakati masoko ya Iringa na Dar es Salaam linauzwa kwa Sh45,000.
- Bei inayotumika leo Mtwara ni zaidi ya mara mbili ya bei ya Iringa na Dar es Salaam, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo.
- Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoa wa Mtwara linauzwa kwa Sh110,000, wakati masoko ya Iringa na Dar es Salaam linauzwa kwa Sh45,000.
Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Mtwara leo watalala na maumivu kutokana na bei ya gunia la kilo 100 la zao hilo kuuzwa zaidi ya mara mbili ya bei inayotumika katika Mikoa ya Iringa na Dar es Salaam na Njombe.
Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Septemba 14, 2020) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Mtwara linauzwa kwa Sh110,000, wakati masoko ya Njombe na Dar es Salaam linauzwa kwa Sh45,000.
Hiyo ina maana kuwa bei inayotumika leo Mtwara ni zaidi ya mara mbili ya Iringa na Dar es Salaam, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo.
Bei hiyo inayotumika Mtwara ndiyo bei ya juu huku ya Iringa na Dar es Salaam ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini.