Huu ndiyo uchungu wa mwana kwa mzazi wake
Wakati mabinti wenzake wanatengeneza mavazi, Enola ni mwana sayansi na mpiganaji.
- Ni filamu inayomhusu mwanadada Enola ambaye amelelewa na mama yake pasi kujua mafunzo ya kuwa binti katika jamii yake.
- Wakati mabinti wenzake wanatengeneza mavazi, Enola ni mwana sayansi na mpiganaji.
- Hata hivyo, uchungu wa mwana kwa mzazi unaingia pichani baada ya mama yake kupotelea kusikojulikana.
Dar es Salaam. Tuanzie wapi? Enola amezaliwa na mama yake! Hahaha, kusimulia hadithi inaweza kuwa changamoto.
Tofauti na wasichana wengine ambao baada ya kuzaliwa hufundishwa kazi ambazo jamii imezitenga maalumu kwa wanawake yaani kupika na kufanya usafi na zinazohusiana na hizo.
Lakini Enola alifundishwa kupigana, michezo na hata kuchangamana na kemikali yaani kuwa mwanasayansi na mengine yote wanayoyafanya wanaume.
Ajabu ni kuwa aliyemfundisha mambo hayo ni mama yake.
Wakati amemzoea mama yake kiasi cha kutokutaka lolote la duniani liwatenganishe, Enola anajikuta hamuoni mama yake. Yaani anaamka na na anamtafuta nyumba nzima na hayupo.
Soma zaidi
- Santana: Filamu itakayokufundisha ubaya wa visasi
- Wanachokiwaza wanaume juu ya mitindo ya nywele za wanawake
- Kuwa makini: Serikali yatoa kanuni kudhibiti zaidi maudhui mtandaoni Tanzania
Safari ya kumtafuta mzazi wake inaanza kwa kutaka kuungana na kaka zake ambao huenda jina la mmoja wao linaweza kugonga kengere masikioni mwako.
Sherlock Holmes. Ndiyo! Askari mpelelezi anayesifika dunia nzima kwa uwezo wake wa kunusa tukio la uhalifu na kulitatua hata pale dunia nzima inaposhindwa.
Sherlock ambaye anaambatana na Mycroft Holmes hawana ujanja bali kumpokea Enola Holmes ambaye ni binti asiyejua jinsi ya kuwa binti kwenye jamii ya Waingereza.
Je, watafanikiwa kumpata mama yake na Enola? Fuatilia filamu ya Enola Holmes kwa mikasa na vitimbwi vya kuvunja mbavu kupitia mtandao wa Netflix ifikapo Septemba23 2020.