November 24, 2024

Wasichana vinara masomo ya sayansi kidato cha sita 2020

Ufaulu wa wasichana umekuwa bora kuliko wa wavulana kwa takriban asilimia moja

  • Ufaulu wa wasichana umekuwa bora kuliko wa wavulana kwa takriban asilimia moja. 
  • Kati ya wasichana hao 10 bora, watatu wametoka St. Mary’s Mazinde juu

Nani alisema masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wanaume? Kwa wasichana hawa ndoto zao zimetimia na wanavunja nadhari kuwa sayansi ni wavulana pekee. 

Huenda baadhi ya wanafunzi hawa walitarajia matokeo hayo lakini kwa kifupi wote na wasiotarajia wameingia kwenye orodha ya wanafunzi 10 wasichana bora katika masomo ya sayansi kitaifa katika mitihani ya kidato cha sita iliyofanywa hivi karibuni. 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, wakati akitangaza matokeo ya mithani  Ijumaa ya Agosti 21, 2020, amewaambia wanahabari Zanzibar kuwa Maria Gambaloya kutoka Marian Girls’ ndiye msichana bora kwa masomo ya sayansi kitaifa akifuatiwa na Marietha Mondea kutoka St. Mary’s Mazinde Juu.

Dk Msonde amebainisha  kuwa ubora wa ufaulu wa wasichana kwa mwaka 2020 ni mzuri zaidi kuliko wa wavulana kwa asilimia 0.89



Kati ya 10 bora hiyo katika masomo ya sayansi, watatu wanatoka Shule ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga, wawili kutoka Shule ya Marian Girls’ iliyopo mkoani Pwani, wawili kutoka Shule ya Feza Girls’ iliyopo mkoani Dar es Salaam na wengine kutoka mikoa ya Mwanza, Tabora na Mbeya

Hawa ndiyo wasichana walioingia 10 bora masomo ya sayansi mitihani ya kidato cha sita 2020.

  1. Maria Hewa Gambaloya (PCM) – Marian Girls’.
  2. Marietha Pastory Mondea (PCM) – St. Mary’s Mazinde Juu
  3. Nisha. B Nkya (PCM) – Feza Girls’
  4. Clara Fredy Malando (PCB) – Tabora Girls’
  5. Elizabeth Mangu (PCM) – Marian Girls’ 
  6. Rosemary. L Kilembe (PCM) – Feza Girls’
  7. Anna Peter Mlay (PCM) – Panda Hill
  8. Elizabeth. B Kway (PCM) – St. Mary’s Mazinde Juu
  9. Elizabeth Lucas Ngwalu (PCM) – St. Mary’s Mazinde Juu
  10. Carolina Sijaona Kabebeka (PCM) – Nganza