October 7, 2024

Jinsi ya kuthibitisha habari za Corona unapotumia Twitter

Ni kwa kutumia programu tumishi ya Twitonomy kujua tabia ya akunti ya Twitter unayotilia mashaka kuhusu Corona.

  • Ni kwa kutumia programu tumishi ya Twitonomy kujua tabia ya akunti ya Twitter unayotilia mashaka.
  • Itakusaidia kufahamu aina ya habari zinazochapishwa kama ni za kweli. 
  • Wakati mwingine programu hiyo inaweza isikupe matokeo unayoyahitaji. 

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa Twitter na umekuwa ukikutana na akaunti ambazo una mashaka nazo kwa sababu zimekuwa zikitumika kupotosha kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona, basi usiwaze sana maana suluhisho lipo. 

Njia rahisi ya kufahamu akaunti feki na zinazozusha kuhusu habari za uongo zikiwemo za Corona ni kutumia programu tumishi ya Twitonomy ambayo inasaidia kufuatilia kwa ukaribu akaunti husika ili kujiweka salama dhidi ya madhara ya habari hizo. 

Twitonomy ni zana ya kidijitali au programu ambayo hutumika kuchambua akaunti za mtandao wa kijamii wa Twitter pale unapohisi akaunti imekuwa ni chanzo cha kusambaza habari za uzushi mtandaoni.


Zinazohusiana:


Twitonomy inamuwezesha mtumiaji kujua tabia za akaunti anayoitilia mashaka ikiwemo inachapisha habari mara ngapi, nyakati gani, wafausi wake ni akina nani na inachapisha nini, ingawa matokea haya yanaweza yasiwe kwa asilimia 100.

Kitendo cha kuweza kujua tu tabia ya akunti hiyo ya Twitter itakuepusha na madhara yatokanayo na habari za uzushi. Pia ni njia rahisi ya kufahamu kama akaunti inamilikiwa na mtu au roboti. 

Kumbuka Twitonomy ni zana inayotumika unapofanya kazi za uthibitishaji habari lakini wakati mwingine inaweza isikupe matokeo unayoyahitaji kwa kiwango cha asilimia 100.