Mboga za majani hazitibu ugonjwa wa Corona
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema ni kweli mboga za majani zinaongeza kinga lakini mboga mboga hizo hazitibu ugonjwa wa corona.
- Mpaka sasa hakuna kinga wala tiba ya kutibu corona
- Mboga hizo ni muhimu kwa kinga ya mwili lakini siyo tiba ya Corona.
Dar es Salaam. Licha ya kuwa mboga za majani kuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa mwili wa mwanadamu, baadhi ya wanaamini kuwa ulaji wa mboga hizo unaweza kutibu ugonjwa wa virusi vya Corona, jambo siyo kweli.
Huenda na wewe ni miongoni mwa watu ambao wanaamini hivyo baada ya kupata habari hizo mtandaoni ukiwemo wa mtandao wa Opera News ambao uliripoti hivi karibuni kuwa “COVID-19 cure revealed: Eat this popular vegetable and never be a victim of coronavirus”
Kwa tafsiri isiyo rasmi habari hiyo inaeleza kuwa : Imebainika kuwa COVID-19 inatibika: Kula mboga hizi za majani maarufu ili usiwe mwathirika wa virusi vya Corona. Mboga ambazo zimetajwa na habari hiyo ni pamoja na ulaji wa bamia na spinachi ili kuweza kujinga na Corona.
Zinazohusiana.
- Picha za tetemeko Croatia zilivyotumika kupotosha Corona mtandaoni
- Siyo kweli wananchi Italia wanatupa pesa mitaani kuepuka Corona
Ukweli Ukoje
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema ni kweli mboga za majani zinaongeza kinga lakini mboga mboga hizo hazitibu ugonjwa wa corona.
Pia kupitia mtandao wa Shirika hilo kwenye kipengele cha maswali na majibu limesema mpaka sasa hakuna matibabu ya ugonjwa wa corona lakini dalili zinazotokana na ugonjwa huo zinaweza kutibika.
Wakati huo huo msemaji wa WHO Tarik Jasarevic ameimbia taasisi ya kuthistisha habari ya Afrika Mashariki ya Pesa Check kuwa hakuna kinga ya corona na hakuna chakula kinachoweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Watu wanasisitizwa kuendelea kujikinga kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.