October 7, 2024

Google inavyowezesha uthibitishaji wa taarifa za Corona mtandaoni

Utaweza kutafuta habari zilizothibitishwa za corona duniani kwa njia mbalimbali ikiwemo jina la chombo cha habari au lugha .

  • Imetengeneza zana ya kidijitali ya “Fact Check Tools” ambayo inasaidia kufahamu habari zilizothibitishwa mtandaoni.
  • Utaweza kutafuta habari zilizothibitishwa za corona duniani kwa njia mbalimbali ikiwemo jina la chombo cha habari au lugha .

Dar es Salaam.Kama wewe ni mwandishi wa habari, mtafiti au mthibitishaji habari umekuwa ikitafuta zana za kidijitali zitakazokusaidia kuthibitisha habari wakati huu wa janga la Corona na bado hujafanikiwa, basi usihofu maana suluhisho limepatikana.

Kampuni ya teknolojia ya Google imetengeneza zana ya kuthibitisha ukweli inayojulikana kama “Fact Check Tools” ambayo inasaidia kufahamu habari zilizothibitishwa mtandaoni.

Kazi yake kubwa ni kuweza kukusanya habari zote zilizothibitishwa na taasisi uthibitishaji wa habari za uzushi duniani katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Ili kuweza kuitumia zana hiyo mtumiaji atatakiwa kwenda kwenye kitafutio cha Google na kutafuta neno “Fact Check Tools” kisha atapata majibu ambayo yatampeleka moja kwa moja kwenye zana hiyo husika.


Zinazohusiana


Ingawa mtandao wa Google umetoa angalizo kuwa hauhusiki moja kwa moja na habari hizo kama utakuwa na jambo lolote kuhusu habari hiyo utawajibika kutafuta wamiliki wa tovuti waliothibitisha taarifa husika.

Jinisi ya kutumia

Hatua inayofuata baada ya kuipata zana hiyo, mtumiaji ataweza kutafuta habari yoyote iliyothibitishwa kuhusu Corona.

Habari hizo zimethibitishwa na  wathitishwa wengi kutoka katika taasisi kubwa ulimwenguni kama Shirika la Habari la AFP, kampuni ya Boom kutoka nchini India na PolitiFact.

Mwanahabri au mdau yoyote anayetaka kufanya habari kuhusu uthibitisha ataweza kuitafuta kwa kuandika kichwa  cha habari  husika au kwa kubonyeza kiunganishi (link) ambacho kipo chini ya zana hiyo ambapo kiunganishi hicho kitakupa habari zilizothibitishwa za siku za karibuni (Recent Fact checks)

Pia anaweza kutafuta habari kwa kutumia jina la wathitishaji au chombo husika cha habari na kupata kwa lugha unayotaka.