October 7, 2024

Robo ya bajeti ya 2020-21 kulipa deni la Serikali

Sh10.48 trilioni sawa na theluthi moja zitaelekezwa katika kulipa deni la Serikali.

  • Sh10.48 trilioni sawa na theluthi moja au robo zitaelekezwa katika kulipa deni la Serikali.

Dar es Salaam. Licha ya Serikali kutenga bajeti ya Sh34.88 kwa mwaka fedha wa 2020/21, robo ya bajeti hiyo itatumika kulipa deni la Serikali. 

Katika mgawanyo wa matumizi ya bajeti hiyo ambayo utekelezaji wake utaanza Julai 1 mwaka huu, Sh10.48 trilioni sawa na theluthi moja au robo zitaelekezwa katika kulipa deni la Serikali. 

Wakati deni la Serikali likitengewa asilimia 25 ya bajeti hiyo, shughuli za maendeleo ndiyo zimetengewa kiasi kikubwa cha fedha cha Sh12.78 trilioni, ambayo ni sawa na asilimia 37 ya bajeti yote.

Kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh2.10 trilioni ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge; Sh1.60 trilioni ni kwa ajili ya mradi wa kufua umeme Mto Rufiji; Sh823.7 bilioni ni kwa ajili ya mifuko ya reli, maji na Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Sh490 bilioni ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu; na Sh298.1 bilioni kwa ajili ya elimumsingi bila ada.