Magufuli afanya uteuzi Makatibu Wakuu wizara mbili
Uteuzi huo umemaweka watumishi watatu kwenye nafasi mpya seerikalini.
- Amemteua Prof. Mchembe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya akichukua nafasi ya Dk Zainab Chaula.
- Dk Chaula ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
- Pia Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto akichukua nafasi ya Dk Zainab Chaula ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano iliyotolewa leo (Aprili 22, 2020) inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Prof. Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya.
Dk Chaula amechukua nafasi ya Katibu Mkuu wa Mawasiliano iliyoachwa na mtangulizi wake Dk Maria Sasabo amestaafu.
Zinazohusiana
- Rais Magufuli asema Uchaguzi Mkuu hautaihirishwa
- Maagizo makuu 3 ya Rais Magufuli kwa watendaji serikalini
- Rais Magufuli ateua Mwenyekiti mpya Bodi ya uwekezaji wa mapato ya mafuta na gesi
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo, Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Bakari Kambi ambaye amestaafu.
“Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 22 Aprili, 2020,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa.