November 24, 2024

Wagonjwa wa Corona wafikia 24 Tanzania

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuna ongezeko la wagonjwa wengine wanne wa Corona kutoka Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufikia 24 tangu ulipoingia nchini ka

  • Visa vingine vingine vinne vimethibitishwa leo na Wizara ya Afya.
  • Wagonjwa hao wako Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar. 
  • Serikali yawataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga. 

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuna ongezeko la wagonjwa wengine wanne wa Corona kutoka Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufikia 24 tangu ulipoingia nchini katikati ya Machi 2020. 

Mwalimu wameeleza katika taarifa yake leo (Aprili 6, 2020) kuwa wagonjwa hawo ni pamoja na wagonjwa wawili waliotolewa taarifa jana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kati ya wagonjwa wapya wawili, Mwalimu amesema mmoja ni mwanaume (41), Mtanzania na mfanyabiashara mkazi wa Mwanza aliyeingia nchini akitokea Dubai Machi 24, 2020 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Machi 29 alielekea Mwanza ambapo alichukuliwa vipimo na kukutwa na maambukizi ya Corona.

Mgonjwa huo anauingiza Mwanza katika orodha ya mikoa iliyorekodi wagonjwa wa virusi vya corona hadi sasa ukiwemo mkoa wa jirani wa Kagera.  

“Mgonjwa mwingine ni mwanaume mwenye umri wa miaka 35, raia wa Tanzania mkazi wa Dar es Salaam, mfanyabiashara.

“Wagonjwa wote wako chini ya uangalizi wa watoa huduma za afya katika vituo maalum vya tiba Dar es Salam, Mwanza na Zanzibar,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Zinazohusiana


Aidha, Wizara ya Afya imesema inaendelea kuwafuatilia kwa karibu watu wote waliowahi kukutana na watu hao ili kudhibiti maambukizi mapya ya Corona. 

Mpaka sasa Tanzania imethibitisha kifo cha mtu mmoja aliyefariki kwa ugonjwa huo huku watatu akipona.

Hata hivyo, wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara, kutokugusa pua, mdomo au macho, kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.