October 6, 2024

Bei ya mahindi yashuka

Bei ya juu ya mahindi inayotumika leo katika Mkoa wa Lindi imeshuka kwa Sh5,000 hadi Sh115,000 kutoka 120,000 iliyorekodiwa Ijumaa Machi 20, 2020.

  • Bei ya juu ya mahindi inayotumika leo katika Mkoa wa Lindi imeshuka kwa Sh5,000 hadi Sh115,000 kutoka 120,000 iliyorekodiwa Ijumaa Machi 20, 2020.

Dar es Salaam. Bei ya juu ya mahindi inayotumika leo katika Mkoa wa Lindi imeshuka kwa Sh5,000 hadi Sh115,000 kutoka 120,000 iliyorekodiwa Ijumaa Machi 20, 2020.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Machi 23, 2020) zinaonyesha kuwa gunia la kilo 100 la mahindi linauzwa kwa Sh115,000 katika mkoa huo 

Bei hiyo inayotumika katika masoko ya mkoa huo ndiyo bei ya juu kabisa nchini Tanzania, jambo linalowafaidisha wafanyabiashara waliopeleka zao hilo katika mkoa huo wa kusini mwa Tanzania japokuwa bei imeshuka kidogo. 

Bei hiyo inayotumika leo imeshuka kidogo kutoka 120,000 iliyotumika Ijumaa Machi 20, 2020, jambo linalowafanya wafanyabiashara hao wapoteze Sh5,000 kwa kila gunia la kilo 100. 

Hata hivyo, wenzao wa Musoma mkoani Mara, gunia hilo hilo la kilo 100 wanauza kwa Sh45,000 ikiwa ni pungufu zaidi ya mara mbili ya bei inayotumika Lindi. 

Bei hiyo inayotumika Mara ndiyo bei ya chini kabisa ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Mahindi ni zao linalotegemewa na kaya nyingi nchini Tanzania kwa chakula.