October 6, 2024

Tanzania yateua wawili kuiwakilisha katika kampuni ya madini ya Twiga

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amewateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ya Tanzania katika vikao vya maamuzi vya Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni mpya ya madini ya Twiga.

  • Imewateua wa Casmir Sumba Kyuki na Michael Jonathan Kambi watakaoingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni hiyo. 
  • Kampuni hiyo  (Twiga Minerals Corporation Limited) inamilikiwa na Serikali ya Tanzania  na Kampuni ya madini ya Barrick Gold.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip  Mpango amewateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ya Tanzania katika vikao vya maamuzi vya Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni mpya ya madini ya Twiga.  

Kampuni hiyo  (Twiga Minerals Corporation Limited) inamilikiwa na Serikali ya Tanzania  na Kampuni ya madini ya Barrick Gold.

Taarifa ya Wizara ya Fedha na Mipango iliyotolewa jana (Machi 22, 2020) imeeleza kuwa wajumbe wa walioteuliwa ni Casmir Sumba Kyuki na Michael Jonathan Kambi.

“Uteuzi wa wajumbe hao unaanza leo tarehe 22 Machi 2020,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja.


Soma zaidi:


Uteuzi wa wajumbe hao watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu, unafuatia makubaliano mapya ya namna ya kuendesha kampuni hiyo kwa ubia, yaliyofikiwa kati ya Serikali na Barrick Gold, na kutiwa saini Januari 24, 2020, Jijini Dar Es Salaam.

Kampuni ya Madini ya Twiga inasimamia migodi mitatu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu ambapo Barrick Gold inamiliki asilimia 84 ya hisa na Serikali ya Tanzania inamiliki hisa asilimia 16.