October 6, 2024

Bei ya viazi mviringo haikamatiki Lindi

Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

  • Bei inayotumika leo Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 
  • Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Lindi leo watalala na maumivu kutokana na bei ya gunia la kilo 100 la zao hilo kuuzwa mara nne zaidi ya bei inayotumika katika Mkoa wa Njombe. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na WIzara ya Viwanda na Biashara  leo (Machi 20, 2020) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Hiyo ina maana kuwa bei inayotumika leo Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 

Bei hiyo inayotumika Lindi ndiyo bei ya juu huku ya Njombe ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini.