November 24, 2024

Unataka kujua kusudi lako la kuishi? Tazama filamu hii

Ni filamu ya “The Call of The Wild” inayoonyeshwa wiki katika kumbi za sinema Tanzania. Inasimulia kisa cha mbwa aitwaye “Buck” anayetenganishwa na familia yake lakini baadaye anakuja kutambua kusudi lake.

  • Ni filamu ya “The Call of The Wild” inayoonyeshwa wiki katika kumbi za sinema Tanzania.
  • Inasimulia kisa cha mbwa aitwaye “Buck” anayetenganishwa na familia yake.
  • Safari ya Buck inamfikisha katika kujitambua na kutafuta upendo binafsi.

Dar es Salaam. Kwa wafugaji wote, ni dhahiri kuwa wanakubaliana na msemo unaosema hakuna mnyama ambaye ni mwaminifu kama mbwa.

Kupitia filamu ya “The Call of The Wild”, msemo huo unadhihirishwa kwa vitendo.

Ipo hivi, Buck ambaye yuko kwenye jamii ya mbwa ambao chimbuko lake ni Scotland nchini Uingereza (Scotch Collie) anafungiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi huko California, Marekani.

Akiwa nje ya nyumba hiyo, anaishia kutekwa na kusafirishwa hadi kwenye msitu wa Yukon nchini Canada ambapo anauzwa na kuanza safari mpya ya maisha yake.

Kukutana na John Thornton (Harrison Ford) kunamsogeza karibu na kuitafuta dhamira ya maisha yake na zaidi kujitegemea kwani hapo awali, alikuwa mali ya mtu.

Kwenye ardhi ngeni iliyojaa wanyama pori wageni machoni mwake, Buck ataweza kustahimili na kulifahamu kusudi lake maisha?


Zinazohusiana:


Fuatilia filamu hii ambayo ni riwaya iliyoandikwa na Jack London inayopatikana katika kitabu cha “The Call of The Wild” cha mwaka 1903 ambayo kwa bajeti inayokadiliwa kufikia  Sh346.6 bilioni, imegeuzwa kuwa filamu iliyoongozwa na Chris Sanders ambaye ameongoza zaidi ya filamu 10 zikiwemo “How to Train Your Dragon” na “The Croods”.

Weka Sh10,000 kwa ajili ya kutazama filamu hii itakayokufunza kutafuta kusudi lako la maisha zaidi furaha ya kweli ni ipi kupitia kumbi za kutazamia filamu za Century Cinemax zilizopo kwenye maduka makubwa yakiwemo ya Aura mall na Mlimani city jijini Dar es Salaam.