October 6, 2024

Fursa zilizojificha matumizi ya intaneti Tanzania

Kwa mujibu takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za mwaka 2018, idadi ya watumiaji wa intaneti imefikia milioni 23.1 mwaka juzi kutoka watumiaji wapatao milioni 9.3 waliokuwepo mwaka 2013

Dar es Salaam. Matumizi ya intaneti yanazidi kuongezeka kila mwaka Tanzania na kufungua fursa mbalimbali za mtandaoni ambazo zikitumiwa vizuri zinawaweza kuboresha maisha ya jamii na watu wake. 

Kwa mujibu takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za mwaka 2018, idadi ya watumiaji wa intaneti imefikia milioni 23.1 mwaka juzi kutoka watumiaji wapatao milioni 9.3 waliokuwepo mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara mbili katika kipindi hicho. 

Fursa zinazoambatana na matumizi sahihi hasa kwa vijana ni pamoja na ukuaji wa biashara ya mtandaoni, kurahisisha mawasiliano na utunzaji wa vitu mtandaoni.