November 24, 2024

Yakushangaza shule za mwisho kitaifa matokeo kidato cha nne 2019

Shule ya Kipoke ya mkoani Mbeya imeporomoka kwa kasi kutoka nafasi ya 737 iliyoshika mwaka 2018 hadi nafasi ya mwisho kitaifa mwaka jana.

  • Shule saba katika orodha hiyo zinatoka Zanzibar.
  • Wanafunzi watatu tu walioshirikia mtihani kutoka shule hizo ndiyo walipata daraja la kwanza.
  • Shule ya Kipoke ya mkoani Mbeya imeporomoka kwa kasi kutoka nafasi ya 737 iliyoshika mwaka 2018 hadi nafasi ya mwisho kitaifa mwaka jana.

Dar es Salaam. Matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) hivi karibu yanaonyesha shule za Zanzibar zimeshindwa kujinasua katika orodha ya shule 10 za mwisho kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019, baada ya kuingiza shule saba katika orodha hiyo.

Wanafunzi 1,248 walifanya mtihani huo kutoka katika shule hizo 10 lakini ni  wanafunzi watatu tu ndiyo walipata daraja la kwanza na wote kutoka katika shule mmoja ambayo ilishika mkia kitaifa  ya Kipoke.

Jambo lingine la kushangaza katika orodha hiyo ya shule ya mwisho kitaifa kutoka mkoani Mbeya  imeporomoka kwa kasi kutoka nafasi ya 737 iliyoshika mwaka 2018 hadi nafasi ya mwisho kitaifa mwaka jana.