October 8, 2024

Samatta atua Aston Villa

Anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya Uingereza.

  • Anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya Uingereza. 

Dar es Salaam. Klabu ya soka ya Aston Villa ya nchini Uingereza imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta (27) kutoka Klabu ya  KRC Genrk ya Ubeligiji ameingia kandarasi  ya miaka minne na nusu na klabu hiyo.

Haikuwa  kazi nyepesi kwa kijana kutoka wilayani Temeke katika jiji la Dar es Salaam mpaka katika jiji la Birmingham nchini Uingereza kufikia hatua hiyo. 

Safari hiyo ilianzia klabu ya Africa lyon mwaka 2018 kisha Klabu ya Simba mwaka 2010 na baadaye aliichezea TP Mazembe ya Congo DRC hadi kufika Genrk na sasa amejiunga na Aston Villa.

Baada ya kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Samatta akinukuliwa na  vyombo vya habari amesema ni hatua kubwa katika kazi yake ya kucheza soka la kulipwa.

“Nimefurahi sana,” amesema Samatta na kuongeza kuwa “ni hatua kubwa kwangu katika kazi yangu. Ni hatua kubwa kwa nchi yangu pia. Kila mtu alikuwa akitafuta Mtanzania kucheza kwenye Ligi Kuu za kimataifa hatimaye nimewatoa kimasomaso.”