October 5, 2024

Tanapa yatoa mwongozo utalii wa baiskeli mbugani

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limetoa mwongozo wa mambo ya kuzingatia unapotaka kutumia usafiri huo pindi unapokuwa kwenye hifadhi zake, ikiwa ni hatua ya kukuhakikishia usalama wako wakati ukifurahia vivutio vya utalii.

  • Baiskeli zinazohitajika ni zile zisizotumia umeme.
  • Mwendeshaji anatakiwa kuwa na vifaa vyote vya usalama ikiwemo kofia.
  • Mtalii anapaswa kuwa na mwongozo wa watalii mwenye uzoefu wa na shughuli hiyo. 

Dar es Salaam. Moja ya usafiri unaoweza kutumika katika kutembelea mbuga mbalimbali za wanyama nchini  ni usafiri wa baiskeli kwa sababu ni rahisi kupita katika maeneo mengi ambayo magari hayawezi kupita.

Pamoja na kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huo katika hifadhi za Taifa nchini, inahitaji mtu kuwa na ujuzi wa namna ya kuendesha usafiri huo ili kustahimili mazingira yaliyopo ndani ya hifadhi.

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limetoa mwongozo wa mambo ya kuzingatia unapotaka kutumia usafiri huo pindi unapokuwa kwenye hifadhi zake, ikiwa ni hatua ya kukuhakikishia usalama wako wakati ukifurahia vivutio vya utalii.

Shirika hilo, limeamua kutoa mwongozo huo baada ya wageni wengi kuvutiwa na usafiri huo wawapo mbugani hasa katika hifadhi za Taifa za Kilimanjaro na Arusha.

Ili kuhakikisha mambo yote yanafanyika vizuri, Tanapa imetoa utaratibu maalum ambao watu wanatakiwa kuufuata.

Aina za baiskeli zinazo hitajika

Waendeshaji wanatakiwa kutumia baiskeli zisizosukumwa na nguvu ya umeme “Non-motorized bikes”, na idadi ya baiskeli zitakazokuwa kwenye msafara itategemea na wageni watakaokuwa wamepata kibali kufanya utalii wa baiskeli. 

Vibali vinavyotakiwa ili mwongozaji watalii pamoja na wageni waweze kutumia usafiri huo ni pamoja na kuwa na leseni kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), awe na rekodi safi, utalaam wa unaoridhisha wa kutumia usafiri huo.


Zinazohusiana:


Tahadhari za kuchukua unapokuwa kwenye hifadhi

Baadhi ya tahadhari za kiafya na kiusalama zinatakiwa kuchukuliwa ni waratibu wote wa usafiri huo, wanatakiwa kutoa vifaa maalum vya usalama ikiwemo kofia maalum, huduma za msaada wa haraka (first aid kit)

Lakini watalii wanaotumia usafiri huo wanatakiwa kujiandikisha wakiwa wanaingia na kutoka kwenye hifadhi ambapo wanaotumia aina yoyote ya kilevi hawatoruhusiwa kuingia katika hifadhi na vilevi hivyo.

Baadhi ya vigezo vinavyohitajika ni pamoja na kutoa taarifa mapema kabla ya kuanza shughuli za uendeshaji hifadhini ili Mratibu wa hifadhi atoa vifaa vinavyohitajika kwa mwendeshaji wa baiskeli. 

Pamoja na kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huo katika hifadhi za Taifa nchini, inahitaji mtu kuwa na ujuzi wa namna ya kuendesha usafiri huo ili kustahimili mazingira yaliyopo ndani ya hifadhi. Picha|Mtandao.

Lakini kila baiskeli itaendeshwa na mtu mmoja. Kama watoto wanatumia usafiri huo watakiwa kusimamiwa na watu wazima na hawapaswi kwenda umbali mrefu.   

Shughuli hizo za uendeshaji baiskeli zinatakiwa kufanyika majira ya siku kuanzia saa 12:30 asubuhi mpaka 12:00 jioni.

Kama ulikuwa unajipanga kutembelea mbuga za wanyama hivi karibuni, basi hifadhi za Kilimanjaro na Arusha zinaweza kuwa sehemu muhimu ya kukamilisha utalii wako wa baiskeli kwa kukupatia mandhari nzuri ya wanyama na mimea.