October 6, 2024

Shule 10 zilizoshika mkia matokeo darasa la saba mwaka 2019

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 na kuitaja Shule ya Msingi Mhezi iliyopo mkoa wa Tanga kushika mkia kitaifa.

  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 na kuitaja Shule ya Msingi Mhezi iliyopo mkoa wa Tanga kushika mkia kitaifa.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 na kuitaja Shule ya Msingi Mhezi iliyopo mkoa wa Tanga kushika mkia kitaifa.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kwa ujumla ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 ikilinganishwa na mwaka jana huku asilimia 81.5 ya watahiniwa 933,369 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Shule zingine tisa zilizoungana na Mhezi katika kundi la shule 10 zilizofanya vibaya mwaka huu ni pamoja na Tandari ya Morogoro, Mgata (Morogoro), Nyachiro(Morogoro) na Mbwei (Tanga). Necta imezitaja shule hizo katika takwimu za matokeo ya mtihani huo kwa shule zenye wanafunzi 40 au zaidi. 

Nyingine ni Kilole (Tanga), Lesoit (Manyara), Lumba(Morogoro), Msansao (Singida) na Kishangazi ya mkoani Tanga. 

Mikoa ya Morogoro na Tanga imetoa shule nne kila moja huku Singida na Manyara zikitoa shule moja moja.