October 6, 2024

Ufanye nini simu yako ikiingia maji?

Hali ya simu kuingiliwa maji imekuwa ikiwasababishia hasara watu wengi hasa kama hawajui wafanye nini mara hali hiyo inapowatokea

  • Mbinu za kuikoa ni pamoja na kuizima, kutoa betri, kuikausha kwa kitambaa kikavu. 
  • Njia hizi zitakusaidia kupunguza madhara zaidi yanayoweza kuidhuru kabisa simu yako. 
  • Kama haijapona kwa njia hizo, ipeleke kwa fundi itengenezwe.

Dar es Salaam. “Nilijikuta barabarani wakati mvua inanyesha na sehemu ya kujikinga na mvua ilikua mbali hivyo nilinyeshewa na simu yangu ililoana. 

“Dakika chache, nilipojaribu kuiwasha, haikuwaka tena,” amesema Regan Busanji, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni mmoja wa watu wengi ambao wamewahi kukumbana na changamoto ya simu zao kuingia maji

Hali hii imekuwa ikiwasababishia hasara watu wengi hasa kama hawajui wafanye nini mara simu inapondumbukia au inapolowa maji. 

Lakini usihofu maana ukipatwa na changamoto hiyo tena utakuwa umepata mbinu za kukusaidia. Kwa kuzingatia hilo, www.nukta.co.tz inakuletea mambo ya kufanya mara simu yako inapoingia maji ili kupunguza madhara na kabla ya kumpelekea fundi:

1. Zima simu yako 

Kama maji yameingia ndani ya simu, unashauriwa kuizima na kama ilikuwa imezima kabla ya kuingia maji basi usiiwashe kabisa. Kufanya hivyo kunasaidia simu yako isipige shoti baada ya kuwepo kwa mchangamano wa umeme na maji.

2. Toa Betri

Betri ndiyo kifaa kinacho sambaza umeme kwenye simu yako, endapo kama simu iliyoloana inakuruhusu kutoa betri, basi fanya hivyo mapema ili kuzuia uwezekano wa shoti. Kwa simu zisizoruhusu kutoa betri kwa haraka, fuata maelekezo yanayofuata kwenye makala hii.

Endapo utafuata maelekezo hayo na simu isiwake, basi peleka simu yako kwa fundi kwa ajili ya matengenezo. Picha| Mtandao

3. Kausha simu yako kwa kitambaa

Fanya kila uwezalo kukausha simu yako katika sehemu zote unazoweza kuzifikia. Kwa kufanya hivyo, utazuia kiasi kikubwa cha maji kufika kwenye vifaa vya ndani vya simu yako baada ya hapo, iweke simu yako mahali pakavu ili ikauke. 

Usikung’ute simu yako kama nguo kwani utafanya maji yafike sehemu ambayo hayajafika.


Zinazohusiana


4. Unaweza kutumia mchele

Mchele uliowekwa kwenye bakuli au kontena unaweza kukusaidia kuiponya simu yako. Ifunike simu yako kwenye mchele ili kuupa nafasi ya kufyonza maji yaliyobaki baada ya kuanika simu yako. 

Fahamu kuwa kuiweka simu juani hakuwezi kuondoa maji yote kwani simu yako inaweza kubaki na mvuke hivyo mchele unafyonza unyevu wote uliobaki kwenye simu yako.

Baada ya kufanya hivyo, ni vyema ukatafuta simu mbadala kwaajili ya kutumia wakati unasubiria simu yako kutengemaa.

Endapo utafuata maelekezo haya na simu isiwake, basi peleka simu yako kwa fundi kwa ajili ya matengenezo zaidi.

Mchele unafanya kazi ya kufyonza maji yote ambayo yameingia kwenye simu hata katika mfumo wa mvuke. Baada yakufanya hivyo, ni vyema ukatafuta simu mbadala kwaajili ya kutumia wakati unasubiria simu yako kutengemaa.

Kama utafuata maelekezo hayo na simu isirudi katika hali ya kawaida, basi peleka simu yako kwa fundi kwa ajili ya matengenezo zaidi.