Air Tanzania yasitisha kwa muda safari za kwenda Afrika Kusini
Serikali imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege nchini Afrika Kusini hadi hali ya usalama wa nchi hiyo itakapokuwa sawa.
- Serikali imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege nchini Afrika Kusini hadi hali ya usalama wa nchi hiyo itakapokuwa sawa.
- Abiria waliokuwa wanatumia ndege za Air Tanzania wataendelea kusafirishwa na ndege zingine.
Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Serikali imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege nchini Afrika Kusini hadi hali ya usalama wa nchi hiyo itakapokuwa sawa.
Mhandisi Kamwele aliyekuwa akizungumza leo (Septemba 5, 2019) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), amesema Serikali haitoiruhusu tena ndege aina ya Airbus A220-300 iliyozuiwa nchini Afrika Kusini kuendelea na safari katika ardhi ya nchi hiyo hadi pale itakapohakikishiwa usalama wake wa kutua na kuruka bila kukamatwa.
“Kwa mujibu wa ratiba ilikua inatakiwa kesho, iruke kurudi Afrika Kusini, lakini nyinyi ni mashahidi kuwa nchi ile kwa sasa kuna fujo. Tutasitisha huduma kwa muda mpaka serikali itakapowasiliana na serikali ya Afrika Kusini, kuhakikisha usalama wa abiria na chombo,” amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesema wakati wakishughulikia fidia juu ya kesi hiyo ambayo Wanasheria wa Tanzania wameshinda, abiria waliokuwa wanatumia ndege za Air Tanzania wataendelea kusafirishwa na ndege zingine hadi hali itakapokuwa shwari.
“Kuna taratibu tulizoanza kufanya ili kuhakikisha kwamba abiria wetu wanaokwenda na kutoka Afrika Kusini watapata huduma na shirika letu la ndege kupitia ndege zingine,” amesema.
Soma zaidi:
Aidha, Waziri huyo amesema ndege iko katika hali nzuri na itaendelea na safari zake kama kawaida baada ya kukugauliwa na watalaam.
“Baada ya ndege kukaa siku nane, leo walianza kuikagua, haina madhara yoyote. Tunatarajia muda wa saa 9:00 itaingia kwenye route (safari) za kawaida na kuanza kuruka,” amebainisha Kamwelwe na kuongeza kuwa, “ndege ipo na safari zitaendelea kama kawaida.”
Amesema wakati wakishughulikia fidia juu ya kesi hiyo ambayo Wanasheria wa Tanzania wameshinda, abiria waliokuwa wanatumia ndege za Air Tanzania wataendelea kusafirishwa na ndege zingine hadi hali itakapokuwa shwari. Picha|Mtandao.
Ndege hiyo ilishikiliwa tangu Agosti 23, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya kuzuiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng kutokana na kesi ya fidia dhidi ya Serikali ya Tanzania iliyofunguliwa na Hermanus Steyn, rais wa Afrika Kusini.
Steyn alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali ambazo zilitaifishwa na Serikali ya Tanzania miaka ya 1980. Baadaye ilikubaliwa alipwe fidia ya dola za Marekani milioni 33 na tayari ameshalipwa dola milioni 20 kati ya hizo.
Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, kwa mujibu wa mkulima huyo Tanzania imeacha kulipa deni hilo, hadi kufikia hatua ya kuomba ndege kushikiliwa ilikuwa moja ya harakati zake za kutaka kumaliziwa deni lake.
Lakini jana mwendo wa saa mbili na nusu usiku, ndege hiyo ilitua nyumbani baada ya Wanasheria wa Tanzania kushinda kesi iliyokuwepo mahakamani.